Native Bible

Nahum 1:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Milima hutikisika mbele yake na vilima huyeyuka. Nchi hutetemeka mbele yake, dunia na wote waishio ndani yake.

Nahum 1:5 in English

Nahum 1:5 · Berean Standard Bible

The mountains quake before Him, and the hills melt away; the earth trembles at His presence— the world and all its dwellers.

Context

3Bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, Bwana hataacha kuadhibu wenye hatia. Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni vumbi la miguu yake. 4Anakemea bahari na kuikausha, anafanya mito yote kukauka. Bashani na Karmeli zinanyauka na maua ya Lebanoni hukauka. 5Milima hutikisika mbele yake na vilima huyeyuka. Nchi hutetemeka mbele yake, dunia na wote waishio ndani yake. 6Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu? Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali? Ghadhabu yake imemiminwa kama moto, na miamba inapasuka mbele zake. 7Bwana ni Mwema, kimbilio wakati wa taabu. Huwatunza wale wanaomtegemea,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.