Nahumu 1:4
Nahum 1:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Anakemea bahari na kuikausha, anafanya mito yote kukauka. Bashani na Karmeli zinanyauka na maua ya Lebanoni hukauka.
Nahum 1:4 in English
Nahum 1:4 · Berean Standard Bible
He rebukes the sea and dries it up; He makes all the rivers run dry. Bashan and Carmel wither, and the flower of Lebanon wilts.
Context
2Bwana ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi;
Bwana hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu.
Bwana hulipiza kisasi juu ya watesi wake,
naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake. 3Bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu,
Bwana hataacha kuadhibu wenye hatia.
Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani,
na mawingu ni vumbi la miguu yake. 4Anakemea bahari na kuikausha,
anafanya mito yote kukauka.
Bashani na Karmeli zinanyauka
na maua ya Lebanoni hukauka. 5Milima hutikisika mbele yake
na vilima huyeyuka.
Nchi hutetemeka mbele yake,
dunia na wote waishio ndani yake. 6Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu?
Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali?
Ghadhabu yake imemiminwa kama moto,
na miamba inapasuka mbele zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.