Native Bible

Mark 8:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

Mark 8:11 in English

Mark 8:11 · Berean Standard Bible

Then the Pharisees came and began to argue with Jesus, testing Him by demanding from Him a sign from heaven.

Context

9Watu waliokula walikuwa wapata 4,000. Akiisha kuwaaga, 10aliingia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda sehemu za Dalmanutha. 11Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 12Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin nawaambieni, hakitapewa ishara yoyote.” 13Kisha akawaacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ngʼambo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.