Marko 11:12
Mark 11:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa.
Mark 11:12 in English
Mark 11:12 · Berean Standard Bible
The next day, when they had left Bethany, Jesus was hungry.
Context
10“Umebarikiwa Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!”
“Hosana kwake yeye aliye juu!” 11Yesu akaingia Yerusalemu na kwenda Hekaluni. Akaangalia kila kitu kilichokuwamo, lakini kwa kuwa ilishakuwa jioni, akaenda zake Bethania pamoja na wale kumi na wawili. 12Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa. 13Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. 14Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.