Native Bible

Mark 11:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.

Mark 11:14 in English

Mark 11:14 · Berean Standard Bible

Then He said to the tree, “May no one ever eat of your fruit again.” And His disciples heard this statement.

Context

12Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa. 13Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. 14Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo. 15Walipofika Yerusalemu, Yesu akaingia katika eneo la Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakinunua na kuuza humo ndani. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, 16wala hakumruhusu mtu yeyote kuchukua bidhaa kupitia ukumbi wa Hekalu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.