Native Bible

Micah 7:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wachunge watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, ambalo linaishi peke yake msituni, katika nchi ya malisho yenye rutuba. Waache walishe katika Bashani na Gileadi kama ilivyokuwa siku za kale.

Micah 7:14 in English

Micah 7:14 · Berean Standard Bible

Shepherd with Your staff Your people, the flock of Your inheritance. They live alone in a woodland, surrounded by pastures.* Let them graze in Bashan and Gilead, as in the days of old.

Context

12Siku hiyo watu watakuja kwako kutoka Ashuru na miji ya Misri, hata kutoka Misri hadi Frati na kutoka bahari hadi bahari na kutoka mlima hadi mlima. 13Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake, kwa sababu ya matunda ya matendo yao. 14Wachunge watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, ambalo linaishi peke yake msituni, katika nchi ya malisho yenye rutuba. Waache walishe katika Bashani na Gileadi kama ilivyokuwa siku za kale. 15“Kama siku zile mlipotoka Misri, nitawaonyesha maajabu yangu.” 16Mataifa yataona na kuaibika, waliondolewa nguvu zao zote. Wataweka mikono yao kwenye vinywa vyao na masikio yao yatakuwa na uziwi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.