Mika 7:15
Micah 7:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kama siku zile mlipotoka Misri, nitawaonyesha maajabu yangu.”
Micah 7:15 in English
Micah 7:15 · Berean Standard Bible
As in the days when you came out of Egypt, I will show My wonders.
Context
13Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake,
kwa sababu ya matunda ya matendo yao. 14Wachunge watu wako kwa fimbo yako,
kundi la urithi wako,
ambalo linaishi peke yake msituni,
katika nchi ya malisho yenye rutuba.
Waache walishe katika Bashani na Gileadi
kama ilivyokuwa siku za kale. 15“Kama siku zile mlipotoka Misri,
nitawaonyesha maajabu yangu.” 16Mataifa yataona na kuaibika,
waliondolewa nguvu zao zote.
Wataweka mikono yao kwenye vinywa vyao
na masikio yao yatakuwa na uziwi. 17Wataramba mavumbi kama nyoka,
kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi.
Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka;
watamgeukia Bwana Mungu wetu kwa hofu
nao watakuogopa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.