Mathayo 23:5
Matthew 23:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao.
Matthew 23:5 in English
Matthew 23:5 · Berean Standard Bible
All their deeds are done for men to see. They broaden their phylacteries and lengthen their tassels.
Context
3hivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. 4Wao hufunga mizigo mikubwa na kuiweka mabegani mwa watu, lakini wao wenyewe hawako radhi hata kuinua kidole ili kuisogeza. 5“Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao. 6Wanapenda kukalia viti vya heshima katika karamu, na vile viti maalum sana katika masinagogi. 7Hupenda kusalimiwa masokoni na kutaka watu wawaite ‘Rabi.’*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.