Native Bible

Matthew 23:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

hivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri.

Matthew 23:3 in English

Matthew 23:3 · Berean Standard Bible

So practice and observe everything they tell you. But do not do what they do, for they do not practice what they preach.

Context

1Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake: 2“Walimu wa sheria na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Mose, 3hivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. 4Wao hufunga mizigo mikubwa na kuiweka mabegani mwa watu, lakini wao wenyewe hawako radhi hata kuinua kidole ili kuisogeza. 5“Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.