Mathayo 12:20
Matthew 12:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde.
Matthew 12:20 in English
Matthew 12:20 · Berean Standard Bible
A bruised reed He will not break, and a smoldering wick He will not extinguish, till He leads justice to victory.
Context
18“Tazama mtumishi wangu niliyemchagua,
mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Nitaweka Roho wangu juu yake,
naye atatangaza haki kwa mataifa. 19Hatagombana wala hatapiga kelele,
wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani. 20Mwanzi uliopondeka hatauvunja,
na utambi unaofuka moshi hatauzima,
mpaka atakapoifanya haki ishinde. 21Katika Jina lake mataifa
wataweka tumaini lao.” 22Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Yesu akamponya, hata akaweza kusema na kuona.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.