Native Bible

Luke 22:65 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi.

Luke 22:65 in English

Luke 22:65 · Berean Standard Bible

And they said many other blasphemous things against Him.

Context

63Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?” 65Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi. 66Kulipopambazuka, baraza la wazee wa watu,* yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao. 67Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo,* tuambie.” Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.