Native Bible

Job 5:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia.

Job 5:21 in English

Job 5:21 · Berean Standard Bible

You will be hidden from the scourge of the tongue, and will not fear havoc when it comes.

Context

19Kutoka majanga sita atakuokoa; naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe. 20Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga. 21Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia. 22Utayacheka maangamizo na njaa, wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa wanyama wakali wa mwituni. 23Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba, nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.