Native Bible

Job 5:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba, nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe.

Job 5:23 in English

Job 5:23 · Berean Standard Bible

For you will have a covenant with the stones of the field, and the wild animals will be at peace with you.

Context

21Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia. 22Utayacheka maangamizo na njaa, wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa wanyama wakali wa mwituni. 23Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba, nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe. 24Utajua ya kwamba hema lako li salama; utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua. 25Utajua ya kuwa watoto wako watakuwa wengi, nao wazao wako wengi kama majani ya nchi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.