Ayubu 42:6
Job 42:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo najidharau mwenyewe, na kutubu katika mavumbi na majivu.”
Job 42:6 in English
Job 42:6 · Berean Standard Bible
Therefore I retract my words, and I repent in dust and ashes.”
Context
4“Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena;
nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’ 5Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,
lakini sasa macho yangu yamekuona. 6Kwa hiyo najidharau mwenyewe,
na kutubu katika mavumbi na majivu.” 7Baada ya Bwana kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu. 8Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.