Ayubu 42:5
Job 42:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona.
Job 42:5 in English
Job 42:5 · Berean Standard Bible
My ears had heard of You, but now my eyes have seen You.
Context
3Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’
Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi,
mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua. 4“Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena;
nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’ 5Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,
lakini sasa macho yangu yamekuona. 6Kwa hiyo najidharau mwenyewe,
na kutubu katika mavumbi na majivu.” 7Baada ya Bwana kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.