Native Bible

Job 4:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; kwa mshindo wa hasira zake huangamia.

Job 4:9 in English

Job 4:9 · Berean Standard Bible

By the breath of God they perish, and by the blast of His anger they are consumed.

Context

7“Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia? Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa? 8Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza, wale walimao ubaya na wale hupanda uovu, huvuna hayo hayo hayo. 9Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; kwa mshindo wa hasira zake huangamia. 10Simba anaweza kunguruma na kukoroma, lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika. 11Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo, nao wana wa simba jike hutawanyika.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.