Ayubu 27:16
Job 27:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,
Job 27:16 in English
Job 27:16 · Berean Standard Bible
Though he heaps up silver like dust and piles up a wardrobe like clay,
Context
14Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani,
fungu lao ni kuuawa kwa upanga;
wazao wake hawatakuwa kamwe
na chakula cha kuwatosha. 15Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao,
nao wajane wao hawatawaombolezea. 16Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi,
na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi, 17yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa,
naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake. 18Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui,
kama kibanda alichotengeneza mlinzi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.