Ayubu 27:17
Job 27:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
Job 27:17 in English
Job 27:17 · Berean Standard Bible
what he lays up, the righteous will wear, and his silver will be divided by the innocent.
Context
15Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao,
nao wajane wao hawatawaombolezea. 16Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi,
na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi, 17yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa,
naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake. 18Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui,
kama kibanda alichotengeneza mlinzi. 19Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho;
afunguapo macho yake, yote yametoweka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.