Native Bible

Job 27:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea.

Job 27:15 in English

Job 27:15 · Berean Standard Bible

His survivors will be buried by the plague, and their widows will not weep for them.

Context

13“Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi: 14Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha. 15Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea. 16Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi, 17yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.