Native Bible

Job 27:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.

Job 27:18 in English

Job 27:18 · Berean Standard Bible

The house he built is like a moth’s cocoon, like a hut set up by a watchman.

Context

16Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi, 17yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake. 18Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi. 19Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka. 20Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.