Ayubu 26:4
Job 26:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo? Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?
Job 26:4 in English
Job 26:4 · Berean Standard Bible
To whom have you uttered these words? And whose spirit spoke through you?
Context
2“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!
Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu! 3Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?
Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha! 4Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?
Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako? 5“Wafu wako katika maumivu makuu,
wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake. 6Mauti* iko wazi mbele za Mungu;
Uharibifu* haukufunikwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.