Native Bible

Job 24:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Huwanyangʼanya yatima punda wao, na kumchukua rehani fahali wa mjane.

Job 24:3 in English

Job 24:3 · Berean Standard Bible

They drive away the donkey of the fatherless and take the widow’s ox in pledge.

Context

1“Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio? 2Watu husogeza mawe ya mpaka; huchunga makundi ya wanyama waliyonyangʼanya kwa nguvu. 3Huwanyangʼanya yatima punda wao, na kumchukua rehani fahali wa mjane. 4Humsukuma mhitaji kutoka njia, na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha. 5Kama punda-mwitu jangwani, maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula; mahali palipo jangwa huwapa chakula cha watoto wao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.