Ayubu 23:13
Job 23:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga? Yeye hufanya lolote atakalo.
Job 23:13 in English
Job 23:13 · Berean Standard Bible
But He is unchangeable, and who can oppose Him? He does what He desires.
Context
11Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu;
nimeishika njia yake bila kukengeuka. 12Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake;
nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku. 13“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga?
Yeye hufanya lolote atakalo. 14Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu,
na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba. 15Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake;
nifikiriapo haya yote ninamwogopa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.