Native Bible

Job 23:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu, na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba.

Job 23:14 in English

Job 23:14 · Berean Standard Bible

For He carries out His decree against me, and He has many such plans.

Context

12Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake; nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku. 13“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga? Yeye hufanya lolote atakalo. 14Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu, na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba. 15Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake; nifikiriapo haya yote ninamwogopa. 16Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia; yeye Mwenyezi amenitia hofu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.