Native Bible

Job 15:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu? Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe?

Job 15:8 in English

Job 15:8 · Berean Standard Bible

Do you listen in on the council of God or limit wisdom to yourself?

Context

6Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu; midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako. 7“Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? Ulizaliwa kabla ya vilima? 8Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu? Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe? 9Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi? Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi? 10Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu, watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.