Native Bible

Jeremiah 51:41 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Tazama jinsi Sheshaki* atakamatwa, majivuno ya dunia yote yatakavyonyakuliwa. Babeli atakuwa mwenye hofu kiasi gani kati ya mataifa!

Jeremiah 51:41 in English

Jeremiah 51:41 · Berean Standard Bible

How Sheshach * has been captured! The praise of all the earth has been seized. What a horror Babylon has become among the nations!

Context

39Lakini wakati wakiwa wameamshwa, nitawaandalia karamu na kuwafanya walewe, ili wapige kelele kwa kicheko, kisha walale milele na wasiamke,” asema Bwana. 40“Nitawateremsha kama wana-kondoo waendao machinjoni, kama kondoo dume na mbuzi. 41“Tazama jinsi Sheshaki* atakamatwa, majivuno ya dunia yote yatakavyonyakuliwa. Babeli atakuwa mwenye hofu kiasi gani kati ya mataifa! 42Bahari itainuka juu ya Babeli; mawimbi yake yenye kunguruma yatamfunika. 43Miji yake itakuwa ukiwa, kame na jangwa, nchi ambayo hakuna yeyote anayeishi ndani yake, ambayo hakuna mtu anayepita humo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.