Native Bible

Jeremiah 51:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Miji yake itakuwa ukiwa, kame na jangwa, nchi ambayo hakuna yeyote anayeishi ndani yake, ambayo hakuna mtu anayepita humo.

Jeremiah 51:43 in English

Jeremiah 51:43 · Berean Standard Bible

Her cities have become a desolation, a dry and arid land, a land where no one lives, where no son of man passes through.

Context

41“Tazama jinsi Sheshaki* atakamatwa, majivuno ya dunia yote yatakavyonyakuliwa. Babeli atakuwa mwenye hofu kiasi gani kati ya mataifa! 42Bahari itainuka juu ya Babeli; mawimbi yake yenye kunguruma yatamfunika. 43Miji yake itakuwa ukiwa, kame na jangwa, nchi ambayo hakuna yeyote anayeishi ndani yake, ambayo hakuna mtu anayepita humo. 44Nitamwadhibu Beli katika Babeli, na kumfanya atapike kile alichokimeza. Mataifa hayatamiminika tena kwake. Nao ukuta wa Babeli utaanguka. 45“Tokeni ndani yake, enyi watu wangu! Okoeni maisha yenu! Ikimbieni hasira kali ya Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.