Native Bible

Jeremiah 51:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo, wanakoroma kama wana simba.

Jeremiah 51:38 in English

Jeremiah 51:38 · Berean Standard Bible

They will roar together like young lions; they will growl like lion cubs.

Context

36Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo: “Tazama, nitatetea shauri lako na kulipiza kisasi kwa ajili yako; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake. 37Babeli utakuwa lundo la magofu na makao ya mbweha, kitu cha kutisha na kudharauliwa, mahali asipoishi mtu. 38Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo, wanakoroma kama wana simba. 39Lakini wakati wakiwa wameamshwa, nitawaandalia karamu na kuwafanya walewe, ili wapige kelele kwa kicheko, kisha walale milele na wasiamke,” asema Bwana. 40“Nitawateremsha kama wana-kondoo waendao machinjoni, kama kondoo dume na mbuzi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.