Yeremia 51:36
Jeremiah 51:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo: “Tazama, nitatetea shauri lako na kulipiza kisasi kwa ajili yako; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake.
Jeremiah 51:36 in English
Jeremiah 51:36 · Berean Standard Bible
Therefore this is what the LORD says: “Behold, I will plead your case and take vengeance on your behalf; I will dry up her sea and make her springs run dry.
Context
34“Nebukadneza mfalme wa Babeli ametula,
ametufanya tuchangayikiwe,
ametufanya tuwe gudulia tupu.
Kama nyoka ametumeza
na kujaza tumbo lake kwa vyakula vyetu vizuri,
kisha akatutapika. 35Jeuri iliyofanyiwa miili yetu* na iwe juu ya Babeli,”
ndivyo wasemavyo wakaao Sayuni.
“Damu yetu na iwe juu ya wale waishio Babeli,”
asema Yerusalemu. 36Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo:
“Tazama, nitatetea shauri lako
na kulipiza kisasi kwa ajili yako;
nitaikausha bahari yake
na kuzikausha chemchemi zake. 37Babeli utakuwa lundo la magofu
na makao ya mbweha,
kitu cha kutisha na kudharauliwa,
mahali asipoishi mtu. 38Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo,
wanakoroma kama wana simba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.