Native Bible

Jeremiah 51:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Babeli utakuwa lundo la magofu na makao ya mbweha, kitu cha kutisha na kudharauliwa, mahali asipoishi mtu.

Jeremiah 51:37 in English

Jeremiah 51:37 · Berean Standard Bible

Babylon will become a heap of rubble, a haunt for jackals,* an object of horror and scorn, without inhabitant.

Context

35Jeuri iliyofanyiwa miili yetu* na iwe juu ya Babeli,” ndivyo wasemavyo wakaao Sayuni. “Damu yetu na iwe juu ya wale waishio Babeli,” asema Yerusalemu. 36Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo: “Tazama, nitatetea shauri lako na kulipiza kisasi kwa ajili yako; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake. 37Babeli utakuwa lundo la magofu na makao ya mbweha, kitu cha kutisha na kudharauliwa, mahali asipoishi mtu. 38Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo, wanakoroma kama wana simba. 39Lakini wakati wakiwa wameamshwa, nitawaandalia karamu na kuwafanya walewe, ili wapige kelele kwa kicheko, kisha walale milele na wasiamke,” asema Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.