Yeremia 51:3
Jeremiah 51:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usimwache mpiga upinde afunge kamba upinde wake, wala usimwache avae silaha zake. Usiwaonee huruma vijana wake; angamiza jeshi lake kabisa.
Jeremiah 51:3 in English
Jeremiah 51:3 · Berean Standard Bible
Do not let the archer bend his bow or put on his armor. Do not spare her young men; devote all her army to destruction!*
Context
1Hili ndilo asemalo Bwana:
“Tazama nitaamsha roho ya mwangamizi
dhidi ya Babeli na watu wakaao Leb-Kamai.* 2Nitawatuma wageni Babeli
kumpepeta na kuiharibu nchi yake;
watampinga kila upande
katika siku ya maafa yake. 3Usimwache mpiga upinde afunge kamba upinde wake,
wala usimwache avae silaha zake.
Usiwaonee huruma vijana wake;
angamiza jeshi lake kabisa. 4Wataanguka waliouawa katika Babeli,
wakiwa na majeraha ya kutisha barabarani zake. 5Kwa maana Israeli na Yuda hawajaachwa
na Mungu wao, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
ingawa nchi yao imejaa uovu
mbele zake yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.