Native Bible

Jeremiah 49:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa nini mji ambao unajulikana haujaachwa, mji ambao ninaupenda?

Jeremiah 49:25 in English

Jeremiah 49:25 · Berean Standard Bible

How is the city of praise not forsaken, the town that brings Me joy?

Context

23Kuhusu Dameski: “Hamathi na Arpadi imetahayarika, kwa kuwa wamesikia habari mbaya. Wamevunjika moyo na wametaabika kama bahari iliyochafuka. 24Dameski amedhoofika, amegeuka na kukimbia, hofu ya ghafula imemkamata sana; amepatwa na uchungu na maumivu, maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 25Kwa nini mji ambao unajulikana haujaachwa, mji ambao ninaupenda? 26Hakika, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; askari wake wote watanyamazishwa siku hiyo,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 27“Nitatia moto kuta za Dameski; utaangamiza ngome za Ben-Hadadi.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.