Native Bible

Jeremiah 48:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea, enyi watu wa Moabu,” asema Bwana.

Jeremiah 48:43 in English

Jeremiah 48:43 · Berean Standard Bible

Terror and pit and snare await you, O dweller of Moab,” declares the LORD.

Context

41Miji itatekwa na ngome zake zitatwaliwa. Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa. 42Moabu ataangamizwa kama taifa kwa sababu amemdharau Bwana. 43Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea, enyi watu wa Moabu,” asema Bwana. 44“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitaletea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema Bwana. 45“Katika kivuli cha Heshboni, wakimbizi wamesimama pasipo msaada, kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni, mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni; unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu, mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.