Native Bible

Jeremiah 48:42 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Moabu ataangamizwa kama taifa kwa sababu amemdharau Bwana.

Jeremiah 48:42 in English

Jeremiah 48:42 · Berean Standard Bible

Moab will be destroyed as a nation because he vaunted himself against the LORD.

Context

40Hili ndilo asemalo Bwana: “Tazama! Tai anashuka chini, akitanda mabawa yake juu ya Moabu. 41Miji itatekwa na ngome zake zitatwaliwa. Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa. 42Moabu ataangamizwa kama taifa kwa sababu amemdharau Bwana. 43Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea, enyi watu wa Moabu,” asema Bwana. 44“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitaletea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.