Yeremia 48:3
Jeremiah 48:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sikiliza kilio kutoka Horonaimu, kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.
Jeremiah 48:3 in English
Jeremiah 48:3 · Berean Standard Bible
A voice cries out from Horonaim: ‘Devastation and great destruction!’
Context
1Kuhusu Moabu:
Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:
“Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa.
Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa;
Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa. 2Moabu haitasifiwa tena;
huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake:
‘Njooni na tuangamize taifa lile.’
Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa;
upanga utakufuatia. 3Sikiliza kilio kutoka Horonaimu,
kilio cha maangamizi makuu na uharibifu. 4Moabu utavunjwa,
wadogo wake watapiga kelele. 5Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi,
wakilia kwa uchungu wanapotembea,
kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu,
kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.