Yeremia 46:25
Jeremiah 46:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi,* na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao.
Jeremiah 46:25 in English
Jeremiah 46:25 · Berean Standard Bible
The LORD of Hosts, the God of Israel, says: “Behold, I am about to punish Amon god of Thebes,* along with Pharaoh, Egypt with her gods and kings, and those who trust in Pharaoh.
Context
23Wataufyeka msitu wake,”
asema Bwana,
“hata kama umesongamana kiasi gani.
Ni wengi kuliko nzige,
hawawezi kuhesabika. 24Binti wa Misri ataaibishwa,
atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.” 25Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi,* na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao. 26Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Bwana. 27“Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,
usifadhaike, ee Israeli.
Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali,
uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.
Yakobo atakuwa tena na amani na salama,
wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.