Native Bible

Jeremiah 46:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli. Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali, uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. Yakobo atakuwa tena na amani na salama, wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu.

Jeremiah 46:27 in English

Jeremiah 46:27 · Berean Standard Bible

But you, O Jacob My servant, do not be afraid, and do not be dismayed, O Israel. For I will surely save you out of a distant place, your descendants from the land of their captivity! Jacob will return to quiet and ease, with no one to make him afraid.

Context

25Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi,* na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao. 26Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Bwana. 27“Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli. Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali, uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. Yakobo atakuwa tena na amani na salama, wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu. 28Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, kwa maana mimi niko pamoja nawe,” asema Bwana. “Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote ambayo miongoni mwake nimekutawanya, sitakuangamiza wewe kabisa. Nitakurudi, lakini kwa haki tu, wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.