Yeremia 46:28
Jeremiah 46:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, kwa maana mimi niko pamoja nawe,” asema Bwana. “Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote ambayo miongoni mwake nimekutawanya, sitakuangamiza wewe kabisa. Nitakurudi, lakini kwa haki tu, wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”
Jeremiah 46:28 in English
Jeremiah 46:28 · Berean Standard Bible
And you, My servant Jacob, do not be afraid, declares the LORD, for I am with you. Though I will completely destroy all the nations to which I have banished you, I will not completely destroy you. Yet I will discipline you justly, and will by no means leave you unpunished.”
Context
26Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Bwana. 27“Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,
usifadhaike, ee Israeli.
Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali,
uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.
Yakobo atakuwa tena na amani na salama,
wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu. 28Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,
kwa maana mimi niko pamoja nawe,”
asema Bwana.
“Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote
ambayo miongoni mwake nimekutawanya,
sitakuangamiza wewe kabisa.
Nitakurudi, lakini kwa haki tu,
wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.