Native Bible

Jeremiah 46:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Binti wa Misri ataaibishwa, atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.”

Jeremiah 46:24 in English

Jeremiah 46:24 · Berean Standard Bible

The Daughter of Egypt will be put to shame; she will be delivered into the hands of the people of the north.”

Context

22Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia kadiri adui anavyowasogelea na majeshi, watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka, kama watu wakatao miti. 23Wataufyeka msitu wake,” asema Bwana, “hata kama umesongamana kiasi gani. Ni wengi kuliko nzige, hawawezi kuhesabika. 24Binti wa Misri ataaibishwa, atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.” 25Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi,* na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao. 26Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.