Yeremia 46:23
Jeremiah 46:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wataufyeka msitu wake,” asema Bwana, “hata kama umesongamana kiasi gani. Ni wengi kuliko nzige, hawawezi kuhesabika.
Jeremiah 46:23 in English
Jeremiah 46:23 · Berean Standard Bible
They will chop down her forest, declares the LORD, dense though it may be, for they are more numerous than locusts; they cannot be counted.
Context
21Askari wake waliokodiwa katika safu zake
wako kama ndama walionenepeshwa.
Wao pia watageuka na kukimbia pamoja,
hawataweza kuhimili vita,
kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao,
wakati wao wa kuadhibiwa. 22Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia
kadiri adui anavyowasogelea na majeshi,
watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka,
kama watu wakatao miti. 23Wataufyeka msitu wake,”
asema Bwana,
“hata kama umesongamana kiasi gani.
Ni wengi kuliko nzige,
hawawezi kuhesabika. 24Binti wa Misri ataaibishwa,
atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.” 25Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi,* na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.