Yeremia 4:27
Jeremiah 4:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivi ndivyo Bwana asemavyo: “Nchi yote itaharibiwa, ingawa sitaiangamiza kabisa.
Jeremiah 4:27 in English
Jeremiah 4:27 · Berean Standard Bible
For this is what the LORD says: “The whole land will be desolate, but I will not finish its destruction.
Context
25Nilitazama, wala watu hawakuwepo;
kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake. 26Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa,
miji yake yote ilikuwa magofu
mbele za Bwana,
mbele ya hasira yake kali. 27Hivi ndivyo Bwana asemavyo:
“Nchi yote itaharibiwa,
ingawa sitaiangamiza kabisa. 28Kwa hiyo dunia itaomboleza
na mbingu zilizo juu zitakuwa giza,
kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma,
nimeamua na wala sitageuka.” 29Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upinde
kila mji unakimbia.
Baadhi wanakimbilia vichakani,
baadhi wanapanda juu ya miamba.
Miji yote imeachwa,
hakuna aishiye ndani yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.