Native Bible

Jeremiah 4:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa, miji yake yote ilikuwa magofu mbele za Bwana, mbele ya hasira yake kali.

Jeremiah 4:26 in English

Jeremiah 4:26 · Berean Standard Bible

I looked, and the fruitful land was a desert. All its cities were torn down before the LORD, before His fierce anger.

Context

24Niliitazama milima, nayo ilikuwa ikitetemeka, vilima vyote vilikuwa vikiyumbayumba. 25Nilitazama, wala watu hawakuwepo; kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake. 26Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa, miji yake yote ilikuwa magofu mbele za Bwana, mbele ya hasira yake kali. 27Hivi ndivyo Bwana asemavyo: “Nchi yote itaharibiwa, ingawa sitaiangamiza kabisa. 28Kwa hiyo dunia itaomboleza na mbingu zilizo juu zitakuwa giza, kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma, nimeamua na wala sitageuka.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.