Yeremia 25:30
Jeremiah 25:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie: “ ‘Bwana atanguruma kutoka juu; atatoa sauti ya ngurumo kutoka makao yake matakatifu na kunguruma kwa nguvu sana dhidi ya nchi yake. Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu, atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani.
Jeremiah 25:30 in English
Jeremiah 25:30 · Berean Standard Bible
So you are to prophesy all these words against them and say to them: ‘The LORD will roar from on high; He will raise His voice from His holy habitation. He will roar loudly over His pasture; like those who tread the grapes, He will call out with a shout against all the inhabitants of the earth.
Context
28Lakini kama wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Ni lazima mnywe! 29Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’ 30“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie:
“ ‘Bwana atanguruma kutoka juu;
atatoa sauti ya ngurumo
kutoka makao yake matakatifu
na kunguruma kwa nguvu sana
dhidi ya nchi yake.
Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu,
atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani. 31Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia,
kwa maana Bwana ataleta mashtaka dhidi ya mataifa;
ataleta hukumu juu ya wanadamu wote
na kuwaua waovu wote,’ ”
asema Bwana. 32Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Tazama! Maafa yanaenea
kutoka taifa moja hadi jingine;
tufani kubwa inainuka
kutoka miisho ya dunia.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.