Yeremia 25:32
Jeremiah 25:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Tazama! Maafa yanaenea kutoka taifa moja hadi jingine; tufani kubwa inainuka kutoka miisho ya dunia.”
Jeremiah 25:32 in English
Jeremiah 25:32 · Berean Standard Bible
This is what the LORD of Hosts says: “Behold! Disaster is spreading from nation to nation; a mighty storm is rising from the ends of the earth.”
Context
30“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie:
“ ‘Bwana atanguruma kutoka juu;
atatoa sauti ya ngurumo
kutoka makao yake matakatifu
na kunguruma kwa nguvu sana
dhidi ya nchi yake.
Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu,
atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani. 31Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia,
kwa maana Bwana ataleta mashtaka dhidi ya mataifa;
ataleta hukumu juu ya wanadamu wote
na kuwaua waovu wote,’ ”
asema Bwana. 32Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Tazama! Maafa yanaenea
kutoka taifa moja hadi jingine;
tufani kubwa inainuka
kutoka miisho ya dunia.” 33Wakati huo, hao waliouawa na Bwana watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi. 34Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji,
mgaagae mavumbini,
ninyi viongozi wa kundi.
Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia;
mtaanguka na kuvunjavunjwa
kama vyombo vizuri vya udongo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.