Yeremia 25:31
Jeremiah 25:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia, kwa maana Bwana ataleta mashtaka dhidi ya mataifa; ataleta hukumu juu ya wanadamu wote na kuwaua waovu wote,’ ” asema Bwana.
Jeremiah 25:31 in English
Jeremiah 25:31 · Berean Standard Bible
The tumult will resound to the ends of the earth because the LORD brings a charge against the nations. He brings judgment on all mankind and puts the wicked to the sword,’” declares the LORD.
Context
29Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’ 30“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie:
“ ‘Bwana atanguruma kutoka juu;
atatoa sauti ya ngurumo
kutoka makao yake matakatifu
na kunguruma kwa nguvu sana
dhidi ya nchi yake.
Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu,
atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani. 31Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia,
kwa maana Bwana ataleta mashtaka dhidi ya mataifa;
ataleta hukumu juu ya wanadamu wote
na kuwaua waovu wote,’ ”
asema Bwana. 32Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Tazama! Maafa yanaenea
kutoka taifa moja hadi jingine;
tufani kubwa inainuka
kutoka miisho ya dunia.” 33Wakati huo, hao waliouawa na Bwana watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.