Yeremia 22:26
Jeremiah 22:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko.
Jeremiah 22:26 in English
Jeremiah 22:26 · Berean Standard Bible
I will hurl you and the mother who gave you birth into another land, where neither of you were born—and there you both will die.
Context
24“Hakika kama niishivyo,” asema Bwana, “hata kama wewe, Yekonia* mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo. 25Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. 26Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. 27Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.” 28Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa,
chungu kilichovunjika,
chombo kisichotakiwa na mtu yeyote?
Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,
na kutupwa kwenye nchi wasioijua?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.