Native Bible

Jeremiah 22:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa, chungu kilichovunjika, chombo kisichotakiwa na mtu yeyote? Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu, na kutupwa kwenye nchi wasioijua?

Jeremiah 22:28 in English

Jeremiah 22:28 · Berean Standard Bible

Is this man Coniah a despised and shattered pot, a jar that no one wants? Why are he and his descendants hurled out and cast into a land they do not know?

Context

26Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. 27Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.” 28Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa, chungu kilichovunjika, chombo kisichotakiwa na mtu yeyote? Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu, na kutupwa kwenye nchi wasioijua? 29Ee nchi, nchi, nchi, sikia neno la Bwana! 30Hili ndilo Bwana asemalo: “Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto, mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote, kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa, wala kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi wala kuendelea kutawala katika Yuda.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.