Native Bible

Jeremiah 22:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Hakika kama niishivyo,” asema Bwana, “hata kama wewe, Yekonia* mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo.

Jeremiah 22:24 in English

Jeremiah 22:24 · Berean Standard Bible

“As surely as I live,” declares the LORD, “even if you, Coniah * son of Jehoiakim king of Judah, were a signet ring on My right hand, I would pull you off.

Context

22Upepo utawaondoa wachungaji wako wote, na wale ulioungana nao wataenda uhamishoni. Kisha utaaibika na kufedheheka kwa sababu ya uovu wako wote. 23Wewe uishiye Lebanoni, wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi, tazama jinsi utakavyoomboleza maumivu makali yatakapokupata, maumivu kama yale ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa! 24“Hakika kama niishivyo,” asema Bwana, “hata kama wewe, Yekonia* mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo. 25Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. 26Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.