Yeremia 22:25
Jeremiah 22:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo.
Jeremiah 22:25 in English
Jeremiah 22:25 · Berean Standard Bible
In fact, I will hand you over to those you dread, who want to take your life—to Nebuchadnezzar king of Babylon and to the Chaldeans.*
Context
23Wewe uishiye Lebanoni,
wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi,
tazama jinsi utakavyoomboleza
maumivu makali yatakapokupata,
maumivu kama yale ya mwanamke
mwenye utungu wa kuzaa! 24“Hakika kama niishivyo,” asema Bwana, “hata kama wewe, Yekonia* mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo. 25Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. 26Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. 27Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.