Native Bible

Jeremiah 2:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu zisizofaa.

Jeremiah 2:8 in English

Jeremiah 2:8 · Berean Standard Bible

The priests did not ask, ‘Where is the LORD?’ The experts in the law no longer knew Me, and the leaders rebelled against Me. The prophets prophesied by Baal and followed useless idols.

Context

6Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’ 7Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu ili mpate kula matunda yake na utajiri wa mazao yake. Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu, na kuufanya urithi wangu chukizo. 8Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu zisizofaa. 9“Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema Bwana. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako. 10Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu* nawe uangalie, tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, uone kama kumekuwepo kitu kama hiki.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.